Pages

Friday, May 18, 2012

MKUTANO WA G8 WAANZA MAREKANI

Rais Baraka Obama wa Marekani akihutubia mkutano wa Mataifa yenye nguvu za kiuchumi duniani.


Rais wa Marekani Baracka Obama akimkaribisha leo katika ikulu ya White House Rais mpya wa Ufaransa, Francois Hollande kabla ya viongozi hao wawili kujiunga na wenzao katika mkutano wa kilele wa nchi tajiri ulimwenguni G8.
      
Rais Obama analenga kuimarisha uhusiano wa Marekani na Ufaransa na kisha kisha kuishinikiza Ulaya kujitahidi zaidi katika kutatua mgogoro wa kiuchumi unaoendelea kushuhudiwa katika eneo hilo.
Francois Hollande, aliyeapishwa mapema wiki hii kama rais mpya wa Ufaransa, tayari ameibua hisia kali kwa kupinga mpango wa Ulaya wa kubana matumizi na kusema kuwa ataviondoa vikosi vya Ufaransa kutoka Afghanistan ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Obama kumhimiza Hollande

Viongozi wanaoziwakilisha nchi za G8 katika mkutano unaopangwa kuanza Camp Dave
Viongozi wanaoziwakilisha nchi za G8 katika mkutanowa kilele unaopangwa kuanza Camp Dave.

Obama mwenye umri wa miaka 50 huenda akautumia mkutano wake wa utangulizi katika ofisi yake kumhimiza Hollande mwenye umri wa miaka 57, Msoshalisti kutathmini upya mipango yake ya Aghanistan ambayo imeiweka Ufaransa katika ratiba ya kuondoka nchini humo mapema kuliko washirika wake wengine wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO.
Lakini viongozi hao wawili ambao wameleezea uungaji mkono wao kwa sera za ukuaji wa kiuchumi barani Ulaya, wanatarajiwa kuwa na msimamo wa pamoja kuhusu mzozo wa madeni unaoukumba ukanda unaotumia sarafu ya euro, ambao huenda ukaugubika mkutano wa mwishoni mwa wiki wa kundi la nchi nane tahiri zaidi ulimwenguni.
Utawala wa Obama ulitumia fedha nyingi kupambana na mdororo wa uchumi wa mwaka wa 2007-2009, na Hollande analenga kuutumua mpango wa kubana matumizi kwa kupitia uwekezaji wa kubuni nafasi zaidi za ajira.
Mkutano wa kilele wa G8 unajiri wakati Wagiriki wakiendelea kuondoa pesa kwenye akaunti zao kutokana na kuongezeka hofu kwua nchi hiyo itaondoka katika kanda ya sarafu ya euro, na masoko ya hisa yameingiwa hofu kuhusu uwezekano wa kuibuka mgogoro mkubwa wa kiuchumi ulaya.
Mzozo wa Ugiriki wazua hofu

Suala la mgogoro wa deni la Ugiriki linatarajiwabkupewa kipau mbele
Suala la mgogoro wa deni la Ugiriki linatarajiwa kupewa kipau mbele.

Obama na maafisa wenginwa Marekani wamewataka maafisa wa Ulaya kufanya juhudi za kuimarisha ukuaji uchumi katika eneo hilo, wakihofia kuwa hali hiyo huenda ikaathiri uchumi wa Marekani na kutishia nafasi za Obama kuchaguliwa zena katika uchaguzi wa tarehe nane Novemba. Ikulu ya White House iliuhamisha mkutano wa G8 hadi Maryland badala ya Chicago, kama njia moja ya kuepuka maandamano wakati Rais wa Urusi Vladimir Putin akitarajiwa kuhudhuria.
Waziri wake Mkuu Dimtry Medvedev atahudhuria badala yake pamoja na wenzake wa G8 wanaohudhuria kwa mara ya kwanza kama vile Francois Holande, Mario Monti wa Italia, na Yoshihiko Noda wa Japan, pamoja na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na Stephen Harper wa Canada. Wengine ni Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Obama wa Marekani, rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barosso, na Rais wa Baraza kuu la Umoja wa Ulaya Herman van Rompuy.
Huo ndio utakaokuwa mkunao mkuwba zaidi wa kilele kuandaliwa katika eneo la Camp Dave ambalo lilijengwa katika miaka ya tisini na linajulikana kama sehemu ya ilikofanyika mazungumzo yaliyopita ya amani ya mashariki ya kati.

No comments:

Post a Comment