Waziri wa ulinzi wa Marekani Bw. Robert Gates.
Jeshi la Marekani linajiandaa kuziondoa ndege zake za kivita kwenye mstari wa mbele wa mapambano yanayoendelea Libya. Duru za Jumuiya ya Kujihami ya NATO zinaeleza kuwa ndege hizo sasa zitashiriki kwenye harakati za usaidizi katika mzozo wa Libya.
Taarifa zinaeleza kuwa wajibu wa kuchangia ndege za kivita zitakazotumiwa kwenye mashambulio ya angani na ardhini unayaangukia mataifa ya Uingereza,Ufaransa na washirika wengine wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO. Akizungumza bungeni wiki iliyopita,Waziri wa Ulinzi, Robert Gates, alieleza kuwa Marekani itachangia pale itakapohitajika.
No comments:
Post a Comment