Pages

Friday, April 20, 2012

MAKINDA AIKATAA HOJA YA KUMPINGA PINDA

Anna Makinda spika wa Bunge aliyeikata hoja kwa vipengele kadhaa vya mwongozo wa bunge

Taarifa za hivi punde kutoka Bungeni Mjini Dodoma,zinaeleza kuwa Kusudio la Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe la kutaka kupiga kura za kuanzishwa kwa mjadala wa kutokuwa na imani na Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda,limepigwa chini na Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda.
Akisoma kanuni za Bunge,Mh. Spika alisema kwa mujibu wa kanuni za Bunge na Katiba ya Nchi,kusudio la kutaka kumuondoa Madarakani Waziri Mkuu kwa kupiga kura ya kutokuwa na Imani nae ambayo ni taarifa ya maandishi inapaswa kuwasilishwa kwake siku 14 kabla ya siku husika.
                                               Mh. Zotto kabwe mwasilisha hoja bungeni

Hivyo kwakuwa ofisi yake haijapata taarifa ya maandishi ju ya zoezi hilo,basi zoezi hilo moja kwa moja litakuwa ni batili, na kwasababu kikao hicho cha Bunge kinatarajiwa kufungwa siku ya jumatatu,basi hakutakuwa na uwezekano wa zoezi hilo kukamilika.
                                      Mh. January Makamba ndiye aliyeomba mwongozo bungeni

Awali Mbunge wa Jimbo la Bumbuli,Mh. January Makamab aliomba muongozo wa Spika kuhusu jambo hilo ndipo Spika,Mh. Anne Makinda akasimama na kutoa ufafanuzi huo.

1 comment:

  1. ndejembi sema na hawa ndugu zako ujinga umezidi ndani ya chama, wanaiba bila haya bwana!

    ReplyDelete