Mnyika akiwa amebebwa juu zaidi na wanachama wa Chadema waliofika wakati wa kesi yake leo.
Moja ya Marafiki wa Mnyika akimpongeza baada ya ushindi wa kesi ya Mnyika.
Mbunge wa jimbo la
ubungo Mhe. John Mnyika (CHADEMA) leo ameibuka kidedea baada ya kushinda kesi ya
kupinga matokeo ya uchaguzi katika jimbo lake iliyokuwa ikimkabili.
Akitoa hukumu ya kesi hiyo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi kwenye uchaguzi huo Bibi Hawa Ngh'umbi Jaji Upendo Msuya alieleza kuwa upande wa mashitaka (mlalamikaji) umeshindwa kuthibitisha madai ya ukiukaji sheria na taratibu zaujumlishaji kura zilizopelekea ushindi wa Mnyika kama ilivyodaiwa na upande wa mashitaka.
Jaji upendo Msuya
alizitupilia mbali hoja nyingine zilizotolewa na mlalamikaji ikiwa ni pamoja na
uingizaji wa computer tano katika chumba cha kuhesabia kura ambazo zilitumiwa na
wasimamizi kujumlishia kura na kuleta mkanganyiko/tofauti ya kura zilizompa
ushindi, Mnyika kuingia na wafuasi wake katika chumba cha majumuisho, utata wa
marekebisho ya kura katika fomu 21B na madai ya kampeni za kashafa na matusi
dhidi ya mlalamikaji zilizoendeshwa na mgombea John Mnyika.
Ushindi wa John Mnyika umeendelea kuiweka CHADEMA kwenye nafasi nzuri za kisiasa bungeni na mitaani hasa kwa kuzingatia rekodi ya kesi nyingi zilizofunguliwa na wagombea wa CCM dhidi ya wabunge wa chama hicho kupigwa chini.
No comments:
Post a Comment