Pages

Friday, January 7, 2011

GHANA YATOA MSIMAMO WAKE KUHUSU MGOGORO WA IVORY COAST

 Rais wa Ghana John Atta Mills anasema nchi yake haitaelemea upande wowote katika mgogoro wa kisiasa wa Ivory Coast na itaiunga mkono serikali yeyote nchini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa, bwana Mills pia alisema Ghana haiungi mkono matumizi ya  kijeshi kumuondoa kiongozi aliyepo madarakani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo.

Matamshi ya kiongozi huyo wa Ghana yanaonekana kudhoofisha uungaji  wa mkono wa kieneo  kwa mpinzani wa bwana Gbagbo, Alassane Ouattara, ambaye nchi nyingi zinamtambua kama mshindi katika uchaguzi wa rais wa mwezi Novemba. ECOWAS inatishia kumuondoa bwana Gbagbo kwa nguvu kama hatokabidhi madaraka kwa bwana Ouattara.

Ivory Coast imekumbwa na matatizo ya kisiasa kwa takriban mwezi mmoja tangu bwana Gbagbo na bwana Ouattara wote walipodai ushindi katika uchaguzi wa Rais.

Katika maendeleo mengine, Canada na Uingereza wamepinga kufkuzwa nchini humo kwa mabalozi wake hatua iliyochukuliwa na serikali ya bwana Gbagb. Nchi zote zinasema bwana Ouattara pekee ndiye mwenye mamlaka ya kufanya maamuzi kama hayo.

Alhamisi Marekani ilizuia mali za bwana Gbagbo, mke wake na washirika wake wa karibu. Afisa mmoja wa wizara ya fedha Adam Szubin, alisema Rais huyo aliyepo madarakani anaendelea  kuonyesha kupuuza  matakwa ya watu wa Ivory Coast.

No comments:

Post a Comment