Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga ataungana na ujumbe wa viongozi wa Afrika Magharibi wanaorejea Cote d'Ivoire kumshawishi kiongozi wa hivi sasa, Laurent Gbagbo kuondoka madarakani kwa amani.
Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Afrika iliyotolewa hii leo,Waziri mkuu Odinga atakwenda Nigeria kukutana na Rais Goodluck Jonathan, alie pia mwenyekiti wa Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS. Siku ya Jumatatu watakutana na Gbagbo na marais wa Benin na Cape Verde nchini Coted'Ivoire.
Umoja wa Afrika unasema kwamba kuwepo kwa Odinga kutasaidia kuimarisha jitihada za kisiasa. Umoja wa Mataifa,umemtambua Alassane Ouattara mshindi wa uchaguzi wa Cote d'Ivoire na hivyo umeidhinisha tangazo la tume ya uchaguzi ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment