Pages

Sunday, January 2, 2011

RAIS WAZAMANI WA ISRAEL APATIKANA NA HATIA

Rais  wa  zamani  wa  Israel Moshe  Katsav  amepatikana   leo  na hatia  ya  makosa  mawili  ya  ubakaji,  ikiwa  ni  kilele  cha   kashfa iliyojitokeza  miaka  minne  iliyopita   ambayo  ililishangaza  taifa  hilo la  Kiyahudi. Rais  huyo  wa  zamani  anakabiliwa  sasa  na  hukumu ya  kwenda  jela  miaka  minane.
Wakati  mahakama  hiyo  mjini  Tel Aviv  ikitoa  hukumu  hiyo, ambapo  pia  imemhukumu  Katsav   kwa  madai  ya  bughdha  za kingono, vitendo  vinavyovuka  mipaka  na  kuzuwia  sheria kuchukua  mkondo  wake, rais  huyo  wa  zamani  mwenye  umri  wa miaka  65  ambaye  alionekana  dhahiri  kufadhaika, alikuwa akinong'ona  tu,  "hapana ,   hapana".
Hukumu  hiyo  inakuja   baada  ya  kuendeshwa  kesi  hiyo  ambayo imechukua   mwaka  mmoja  na  nusu  na  kujumuisha   madai ambayo  ni  ya  kuhuzunisha, yakimuonesha  Katsav  kuwa   ni mbakaji  ambaye  mara  kwa  mara  huwasumbua  wafanyakazi wanawake  katika  ofisi  yake.
Kiongozi  huyo  wa  zamani  wa  nchi  anashutumiwa   kwa  kumbaka mara   mbili  mwanamke  mmoja  ambaye  ametambuliwa  kwa  jina la  "Aleph"  wakati  akiwa    waziri  wa  utalii, na  kuwafanyia usumbufu  kingono  na  kuwabughudhi  wanawake  wengine  wawili wakati  akiwa  rais. Katsav  amesema  kuwa  hana  hatia  wakati wote  wa  uchunguzi  wa  kesi  hiyo  ya  ubakaji  na  usumbufu  wa kingono.
Awali  alikubali  makubaliano  ya  kutoa  maelezo  yake  mahakamani ambayo  yangemfanya  kukubali madai  madogo  madogo  na  kulipa faini  ili  waendesha  mashtaka  watupilie  mbali  madai  ya  ubakaji, lakini  baadaye  alibadili  msimamo  wake,  na  kufanya  makubaliano hayo  kuwa  batili  na  kusema  anataka  kusafisha  jina  lake mahakamani.
Alilazimika  kujiuzulu  kama  rais , akakabidhi  ofisi  kwa  hasimu wake  Shimon  Peres. Katsav  amewashutumu  wahanga  wake  kwamba wanajaribu  kumwendea  kinyume  na  kudai  kuwa   alikuwa  mhanga wa  juhudi  za  kumchafulia  jina  zinazofanywa  na  kundi  la waendesha  mashtaka   na  vyombo  vya  habari bila  ya  yeye  kuweza kujitetea. Mwanawe  wa  kiume  Boaz Katsav, baada  ya  kutolewa  hukumu  hiyo amesema  kuwa  baba  yake  hana  hatia.
Tunataka  kukata  rifaa. Na kwa  msaada  wa   Mwenyezi  Mungu, kila mmoja atatambua  kuwa  baba  yangu  , rais  wa  nane  wa  taifa  la Israel  hana hatia.
Waziri  mkuu  wa Israel, Benjamin  Netanyahu  amesema  kuwa  ni siku  ya  masikitiko  kwa  taifa  la  Israel  na  raia  wake, lakini ameisifu  kesi  hiyo  kuwa  ni  ishara  ya  nguvu  za  mfumo  wa sheria  wa  nchi  hiyo.

No comments:

Post a Comment