Pages

Thursday, April 26, 2012

BALOZI MAAJAR AWAPONGEZA WATANZANIA KWA KUTIMIZA MIAKA 48 YA MUUNGANO.

                 MIAKA 48 YA MUUNGANO WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

                     PONGEZI KWA WATANZANIA WASHIO MAREKANI NA MEXICO.
Napenda kuwapa pongezi Watanzania waishio Marekani na Mexico, tunaposherehekea miaka 48 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kwa niaba yangu binafsi na kwa niaba ya wenzangu hapa ubalozini tanawatakia watanzania wote kheri na fanaka ya siku hii muhimu katika historia ya nchi yetu. Aidha tunaposherehekea sikukuu hii, napenda kutoa wito kwa watanzania wote kuendeleza undugu na mshikamano wetu ili muungano wetu udumu na taifa la Tanzania lizidi kusonga mbele.

Mungu ibariki Tanzania,

Mwanaidi Sinare Maajar
Balozi wa tanzania nchini Marekani na Mexico
Washington, DC.
April 25,2012.

1 comment:

  1. balozi acha unafiki, unaujua muungano wewe? unanisadia nn mimi?

    ReplyDelete