Katika hafla hiyo fupi
iliyohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, Meya Barrett na
Balozi Maaajar walikubaliana kuendeleaza ushirikiano baina ya miji hii miwili,
ulioanzishwa mwaka 2006, na pia kushawishi wawekezaji na wafanya biashara wa ukanda
huu wa Marekani kuwekeza Tanzania.
Mh. balozi mama Maajari siku alipokutana na Meya wa Wisconsin bwana Ryan Skyfe kufuatia mwaliko alioutoa kwa balozi maajar uliokuwa na lengo la kuzitangaza nyanja mbalimbali za kiutalii nchini Tanzania.
Balozi Maajar yuko Jimboni
Wisconsin kwenye ziara ya kikazi ya siku tatu iliyoandaliwa na muasisi wa
ushirikiano wa miji ya Milwaukee na Morogoro Bw. Ryan Skyfe, ambapo anakutana
na taasisi za elimu, biashara na wawekezaji mbalimbali kwa nia ya kuangalia
maeneo ya ushirikiano wenye tija ili kuleta maendeleo kwa manufaa ya wananchi
wa nchi hizo mbili.
Baadhi ya taasisi alizofanya
nao mazungumzo ni Milwaukee Area Technical College walioko kwenye Jimbo la
Wisconsin mjini Milwaukee ambao wamekubali kushirikiana na mojawapo ya chuo cha
Tanzania na kutoa elimu inayolingana na mitaala ya chuo hicho ambacho
kinaongoza kwenye Jimbo hili kwa kutoa elimu ya vitendo kwenye sekta ya nishati
ya umeme inayowasaidia Wamerekani kupata ajira.
Wengine ni Phoenix
Financial & Investment Services walioko Jimbo la Illinois mjini Chicago na
Helios Solar Works walioko Jimbo la Wisconsin Mjini Milwaukee. Balozi Maajar
pia alipata fursa ya kutoa mada kwenye mkutano uliovutia wakuu wa biashara na
wawakilishi wa makampuni wapatao thelathini kutoka kwenye Jimbo la Wisconsin
wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania.
Aidha Balozi Maajar
alitumia fursa hiyo kuirajamu Tanzania na kutangaza fursa mbalimbali zilizopo
baina ya serikali za nchi hizi mbili kwa wananchi wake kuwekeza na kuendeleza
ushirikiano kwa manufaa yao.
Kila mwaka Balozi wa
Tanzania nchini Marekani huandaa ziara
mahsusi kwa ajili ya maafisa wakuu wa makampuni ya kimarekani kutalii Tanzania na kuangalia fursa
za uwekezaji na biashara nchini Tanzania. Ziara hiyo ambayo inachanganya
biashara na utalii (business and leisure) imekuwa mashuhuri sana miongoni mwa
wafanyabiashara wa Kimarekani ambapo mwaka huu inatarajiwa kufanyika tarehe 22
Juni – 02 Julai, 2012.
Balozi Maajar kesho tarehe
21.02.2012 anatarajia kukutana na Gavana wa Jimbo la Wisconsin Mjini Madison na
baadae kuendelea na ziara yake kwenye miji ya La Farge na La Crosse Jimboni
Wisconsin kabla ya kurejea mjini Washington, jimbo la District of Columbia.Wisconsin, Marekani.
20.02.2012
No comments:
Post a Comment